Matokeo ya mechi zakirafiki barani ulaya

Winga Luis Nani akishangalia bao Haki miliki ya picha Google
Image caption Winga Luis Nani akishangalia bao

Mabingwa wa ulaya Ureno wameichapa kichapo cha mabao 5-0 timu ya Gibraltar ,mchezo huu ulikua wa kwanza wa kimataifa kwa timu ya Gibraltar toka wapate nafasi ya wanachama kwa shirikisho la soka duniani Fifa.

Magoli ya Ureno yalifungwa na Luis Nani, aliyefunga mara mbili Joao Cancelo akaongeza bao la tatu, kiungo Bernardo Silva akaongeza bao la nne, beki kisiki K├ępler Ferreira maarufu kama Pepe akihitimisha ushindi huo kwa bao la tano dakika ya 79

Mashetani wekundu Ubelgiji wakapoteza kwa kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Hispania La Roja winga David Silva, akifunga mabao yote mawili katika mchezo huo .

Ugiriki wameibuka na ushindi nyumbani baada ya kuichapa uholanzi kwa mabao 2-1 mabao ya ushindi yalifungwa na Konstantinos Mitroglou na Giannis Gianniotas huku kiungo Georginio Wijnaldum akifungia uholanzi goli pekee.

The Blues Ufaransa, wao wakawaduwaza kikosi cha Italia, the Azzuri kwa kuwachapa kwa mabao 3-1, magoli ya ufaransa yakifungwa na Antony Martial, Olivier Giroud na Layvin Kurzawa huku goli la kufutia machozi la italia likifungwa na Grazziano Pelle.