Wavenezuela waandamana kupinga utawala

Nicolad Maduro Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nicolas Maduro

Maelfu ya watu nchini Venezuela wameshiriki maandamano ya upinzani katika mji mkuu wa Venezuela Caracas.

Wanachama wa upinzani walijitokeza katika maandamano makubwa kwa miaka miwili wakitaka kuondolewa madarakani kwa Rais Nicolas Maduro.

Wanadai kwamba hawataiacha haki yao ya kikatiba kuandamana kwa amani mpaka pale kutakapokuwa na uchaguzi wa amani, wa kidemokrasia wa mabadiliko ya katiba.

Wanamlaumu Rais Nicolas Maduro kuhusiana na uchumi mbaya wa nchi hiyo na kuituhumu pia Tume ya Taifa ya nchi hiyo kwa makusudi kuchelewesha kura ya maoni ambayo ingeweza kufupisha uwepo wake madarakani.

Hata hivyo wafuasi wa Rais Maduro, ambao chama cha Kisoshalisti kimetawala nchi hiyo kwa miaka 17, pia waliandamana kwa idadi kubwa.

Kabla ya kuanza kwa maandamano hayo wanasiasa kadhaa wa upinzani walikamatwa.