Vijana watumia tamasha kuhimiza amani DR Congo

Vijana watumia tamasha kuhimiza amani DR Congo

Vijana kutoka ukanda wa maziwa makuu wamekusanyika kwenye tamasha ya amani maarufu kama Umoja Festival mjini Bukavu, Kivu Kusini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuhimiza kuwepo kwa amani.

Tamasha hili linalenga kudumisha amani na ushirikiano ndani ya vijana wa ukanda huu ukiwemo Burundi, rwanda na DR Congo.

Mwandishi wa BBC wa eneo la mashariki mwa Congo Byobe Malenga ana taarifa zaidi.