Picha zilizogonga vichwa vya habari Afrika: Tarehe 26 Agost hadi 1 Septemba 2016

Baadhi ya picha kutoka Afrika na na za Waafrika kwengineko wiki hii:

Siku ya Ijumaa, wafuasi wa Upinzani nchini Zimbabwe wanaotaka mabadiliko ya sheria za Uchaguzi walichoma vizuizi katika barabara za mji mkuu wa Harare. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Ijumaa, wafuasi wa Upinzani nchini Zimbabwe wanaotaka mabadiliko ya sheria za Uchaguzi walichoma vizuizi katika barabara za mji mkuu wa Harare.
Watu walikongamana katika eneo la Hammamet,kusini mwa Tunis nchini Tunisia siku iliofuata kusherehekea siku ya Hindu Holi ambapo watu hurusha poda ya rangi hewani. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu walikongamana katika eneo la Hammamet,kusini mwa Tunis nchini Tunisia siku iliofuata kusherehekea siku ya Hindu Holi ambapo watu hurusha poda ya rangi hewani.
Siku hiyo hiyo ,raia wa Gabon walipanga foleni ya kupiga kura katika uchaguzi wa urais. Haki miliki ya picha AP
Image caption Siku hiyo hiyo ,raia wa Gabon walipanga foleni ya kupiga kura katika uchaguzi wa urais.
Siku ya pili baadaye walikuwa bado wakisubiri matokeo Haki miliki ya picha Google
Image caption Siku ya pili baadaye walikuwa bado wakisubiri matokeo
Matokeo hatimaye yalitangazwa siku ya Jumatano ambapo rais Ali Bongo aliibuka mshindi kwa uchache wa kura ,hivyobasi kuzua maandamano miongoni mwa wafuasi wa upinzani wanaosema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu. Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Matokeo hatimaye yalitangazwa siku ya Jumatano ambapo rais Ali Bongo aliibuka mshindi kwa uchache wa kura ,hivyobasi kuzua maandamano miongoni mwa wafuasi wa upinzani wanaosema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.
Upande mwengine wa bara Afrika,wasichana nchini Swaziland walishiriki katika densi ya kila mwaka ya Reed katika makao ya mfalme Haki miliki ya picha MUJAHID SAFODIEN
Image caption Upande mwengine wa bara Afrika,wasichana nchini Swaziland walishiriki katika densi ya kila mwaka ya Reed katika makao ya mfalme
Siku hiyohiyo,watu walisubiri Maiduguri,kaskazini mwa Nigeria kwa mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote kuwasili. Haki miliki ya picha Martin Patience
Image caption Siku hiyohiyo,watu walisubiri Maiduguri,kaskazini mwa Nigeria kwa mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote kuwasili.
Aliandamana na mwanamuziki wa mtindo wa Rock Bono ambapo waliambia vyombo vya habari kwamba watoto 50,000 huenda wakafariki kutokana na utapia mlo iwapo Umoja wa mataifa hautapata ufadhili wa kutosha. Haki miliki ya picha Martin Patience
Image caption Aliandamana na mwanamuziki wa mtindo wa Rock Bono ambapo waliambia vyombo vya habari kwamba watoto 50,000 huenda wakafariki kutokana na utapia mlo iwapo Umoja wa mataifa hautapata ufadhili wa kutosha.
Siku iliofuata katika jimbo la Somaliland ,maelfu ya kondoo na mbuzi walikuwa wakisafirishwa nchini Saudia tayari kwa maandalizi ya mahujaji wa kiislamu kuelekea Hajj,ambayo inaanza wiki ijayo. Haki miliki ya picha Ahmed Said Egeh
Image caption Siku iliofuata katika jimbo la Somaliland ,maelfu ya kondoo na mbuzi walikuwa wakisafirishwa nchini Saudia tayari kwa maandalizi ya mahujaji wa kiislamu kuelekea Hajj,ambayo inaanza wiki ijayo.
Siku hiyo hiyo,maboti madogo 20 yaliokolewa ufukweni mwa taifa la Libya likiwa limejaa raia kutoka Somalia na Eritrea,akiwemo mtu mmoja aliyekuwa na mwanawe wa siku tano. Haki miliki ya picha AP
Image caption Siku hiyo hiyo,maboti madogo 20 yaliokolewa ufukweni mwa taifa la Libya yakiwa yamejaa raia kutoka Somalia na Eritrea,akiwemo mtu mmoja aliyekuwa na mwanawe wa siku tano.
Siku iliofuata nchini Sudan,mtoto alisubiri mkutano na wanahabari ambapo mamlaka ya Sudan ilisema kuwa imewakamataa wahamiaji 800 waliokuwa wakisafiri kupitia taifa hilo wakijaribu kuelekea Ulaya. Haki miliki ya picha ASHRAF SHAZLY
Image caption Siku iliofuata nchini Sudan,mtoto alisubiri mkutano na wanahabari ambapo mamlaka ya Sudan ilisema kuwa imewakamataa wahamiaji 800 waliokuwa wakisafiri kupitia taifa hilo wakijaribu kuelekea Ulaya.
Na huko kaskazini mwa Misri,ngamia walikuwa wamepumzika karibu na Piramidi za Giza. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Na huko kaskazini mwa Misri,ngamia walikuwa wamepumzika karibu na Piramidi za Giza.
Siku ya Alhamisi jua lilipatwa katika maeneo mengi ya Afrika ya kati,ikiwemo hapa nyuma ya mnara wa Askari ,jini Dar es salaam Tanzania Haki miliki ya picha DANIEL HAYDUK
Image caption Siku ya Alhamisi jua lilipatwa katika maeneo mengi ya Afrika ya kati,ikiwemo hapa nyuma ya mnara wa Askari ,jini Dar es salaam Tanzania
Kupatwa huko kwa jua huwa hatari kuangalia,kwa hivyo mwanafunzi huyu wa Mbeya ,kusini mwa Tanzania alitumia miwani maalum Haki miliki ya picha Leonard Mubali
Image caption Kupatwa huko kwa jua huwa hatari kuangalia,kwa hivyo mwanafunzi huyu wa Mbeya ,kusini mwa Tanzania alitumia miwani maalum
-Huku raia wakiangalia miale ya kupatwa huko kwa jua katika dimwi la maji. Haki miliki ya picha DANIEL HAYDUK
Image caption -Huku raia wakiangalia miale ya kupatwa huko kwa jua katika dimwi la maji.

Picha hizi ni kwa niaba ya AFP, AP, EPA, Getty Images na Reuters