Dully Sykes alivyobadilisha muziki wa kizazi kipya Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Dully Sykes alivyobadilisha muziki wa kizazi kipya Tanzania

Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania umepitia katika mabadiliko kadhaa mara kwa mara, lakini mabadiliko makubwa ya kukumbukwa ni mwishoni mwa miaka ya 90 muziki huo ulipobadilika kutoka kurap kwenda kuimba.

Dully Sykes wakati huo akiwa na miaka 16 ndiye aliamua kufanya tofauti na wenzake. Karibia miaka 20 baadaye vijana wengi zaidi wamejiunga katika aina hii ya Muziki.

Arnold Kayanda ametuandalia taarifa ifuatayo.