Uchina yaidhinisha mapatano ya Paris kuhusu hali ya hewa

Kiwanda cha Uchina Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchina hutoa kiasi kikubwa zaidi duniani cha gesi yenye madhara makubwa ya CO2, ambayo husababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Bunge la Uchina limeidhinisha makubaliano ya Paris ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani, limeeleza shirika la habari la taifa hilo.

Uchina hutoa kiasi kikubwa zaidi duniani cha gesi yenye madhara makubwa ya CO2, ambayo husababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Uchina na Marekani zinatarajiwa kutangaza kwa pamoja kuidhinishwa kwa makubaliano hayo katika mkutano wa ushirikiano baina ya nchi hizo baadae leo.

Hatua kubwa kuelekea utekelezwaji wa makubaliano haya ilifikiwa mwezi Disemba, ambapo mataifa hayo yalikubaliana kupunguza gesi chafu kwa kiwango cha kuwezesha kupanda kwa joto la dunia kufikia chini ya nyuzi joto 2.

Wajumbe wa kamati ya bunge la taifa la kongresi la watu wa Uchina- China's National People's Congress wameidhinisha "pendekezo la kuchunguza upya na kuidhinisha mapatano ya Paris " Jumamosi asubuhi katika kilele cha wiki nzima cha vikao vya bunge.

Mkataba wa Paris ni mapatano ya kwanza kuwahi kuzingatiwa zaidi miongoni mwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Utekelezwaji wake utakubalika rasmi kisheria baada yakuidhinishwa na nchi 55 zinazozalisha 55% ya hewa ya Kaboni duniani.