Rais Mugabe awaonya mahakimu Zimbabwe

Maandamano ya kupinga uongozi warais Mugabe Zimbabwe
Image caption Maandamano ya kupinga uongozi w arais Mugabe Zimbabwe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amewalaumu mahakimu wanaoruhusu maandamano dhidi ya serikali, ambayo baadae huwa na fujo.

Alisema mahakimu wanadharau amani, na akawaonya kutothubutu kuonesha dharau wanapofikia uamuzi.

Hapo kesho wafuasi wa upinzani watakwenda mahakamani, kupinga amri iliyopiga marufuku maandamano kwa majuma mawili.

Kiongozi mmoja wa upinzani, Tendai Biti, amemshutumu Rais Mugabe, kwamba anajaribu kuwatisha majaji.

Maandamano kadha ya fujo yamefanywa nchini Zimbabwe katika majuma ya karibuni, huku msukosuko wa kiuchumi ukizidi.