Milio ya risasi yasikika gerezani Ethiopia

Ethiopia
Image caption Ethiopia

Ripoti kutoka Ethiopia, zinasema kuwa risasi nyingi zilifyatuliwa Jumamosi kwenye gereza lenye ulinzi mkali, karibu na mji mkuu, Addis Ababa na kuwashwa moto.

Vyombo vya habari vya huko vinasema, watu kama 20 wameuawa, katika gereza la Qilinto, ambalo linazuia wafungwa wa kisiasa.

Kuna ripoti zisemazo kuwa moto huo uliwashwa kusudi na wafungwa, ambao walitaka kutoroka, lakini hayo hayakuthibitishwa.

Ethiopia imeshuhudia wimbi la maandamano ya kupinga serikali katika sehemu kadha za nchi,maandamano yanayofanywa na makabila fulani makuu ya nchi hiyo.