Merkel atikiswa uchaguzi mdogo Ujerumani

Umaarufu wa Bi. Merkel umekuwa wa hati hati tangu aliporuhusu zaidi ya wakimbizi milioni moja kuingia Ujerumani
Image caption Umaarufu wa Bi. Merkel umekuwa wa hati hati tangu aliporuhusu zaidi ya wakimbizi milioni moja kuingia Ujerumani

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameonekana kutikiswa kisiasa huko kaskazini mashariki mwa jimbo la Mecklenburg-Pomerania.

Kura zilizopigwa katika maeneo ya uchaguzi zinaonesha kuwa watu wanapinga wahamiaji, chama cha AfD kimepingana na chama cha Christian Democratic Union cha Bi. Merkel kwa upande mwingine.

Chama cha mrengo wa kushoto kinaonekana kuweka juu kiuchaguzi.

Umaarufu wa Bi. Merkel umekuwa wa hati hati tangu aliporuhusu zaidi ya wakimbizi milioni moja kuingia Ujerumani kwa mwaka uliopita jambo ambalo chama cha AfD linakibagua.

Kura za leo ni kipimo tosha kwake ikiwa ataendelea kusalia madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu wa hapo mwakani.