Kerry kuongoza mazungumzo ya amani katika mkutano wa G20

Umoja wa mataifa umekuwa ukishiriki kusitisha mapigano Syria
Image caption Umoja wa mataifa umekuwa ukishiriki kusitisha mapigano Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, ataongoza mazungumzo na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, kwenye mkutano wa G20 ambapo watajaribu kuhitimisha mpango wa mapigano nchini Syria na kufungua misaada ya kibinadamu.

Umoja wa mataifa umekuwa ukishiriki kusitisha mapigano na kuruhusu misaada kwa jamii, licha ya kuwa na mazungumzo ya muda mrefu yamefanyika,lakini hakuna mpango wa makubaliano kufikiwa.

Waasi walio kwenye mkoa unayoshikiliwa wa Aleppo wanaripoti kuwa wapo chini ya ulinzi na wamezingirwa kwa mara nyingine baada ya vikosi vya serikali kukamata maeneo ya nje kidogo kusini Magharibi mwa wilaya ya Ramouseh siku ya jumapili.