Serikali yavishambulia vikosi vya waasi nchini Syria

Mojawapo ya kambi za kijeshi zilizoshikiliwa na waasi mwezi uliopita
Image caption Mojawapo ya kambi za kijeshi zilizoshikiliwa na waasi mwezi uliopita

Ripoti kutoka Aleppo zinaonyesha kuwa shambulizi kubwa la vikosi vya waasi wanaoungwa mkono na Serikali ya Syria vimelazimishwa kuzingira mji wote unaoshikiliwa na waasi walio upande wa Mashariki mwa mji uliogawanywa.

Wanaharakati wanasema kuwa vikosi vya serikali vimechukua tena kwa kiasi kikubwa mkoa wa Ramousseh ulioko upande wa kusini-magharibi nje kidogo ya Aleppo.

Mkoa huo ulichukuliwa na muungano wa vikosi vya wapiganaji waasi mwezi uliopita.

Ushindi wa waasi ulionekana kuweka shimoni juhudi za serikali kuzingira njia ya mamia wakazi walio upande wa waasi.

Image caption Huduma za miundombinu zimeharibiwa vibaya

Juhudi za wanadiplomasia kumaliza mapigano Aleppo na maeneo mengine ya syria zimegonga huku mazungumzo baina ya Marekani na Urusi yakishindwa kufikia makubaliano ya mwisho.