Utafiti: Kiingereza hutatiza sana wanafunzi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Utafiti: Kiingereza hutatiza sana wanafunzi Tanzania

Nchini Tanzania taasisi ya utafiti wa masuala ya elimu Twaweza imetoa ripoti yake inayoonesha kuwa asilimia 44 ya wanafunzi wanaomaliza shule za msingi nchini Tanzania hawajui kusoma vitabu vya Kiingereza vya darasa la pili.

Hata hivyo kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 16 wamebainika kuwa nao hawawezi kusoma vitabu vya Kiswahili vya darasa la pili.

Kutoka Dar es Salaam Mwandishi Munira Hussein ametuandalia taarifa ifuatayo.