Mfano wa London 1666 ulioteketezwa katika Mto Thames
Huwezi kusikiliza tena

'London yateketea': Mfano wa mji wateketezwa kukumbuka moto wa 1666

Mfano wa jiji la London lilivyokuwa mwaka 1666 umeteketezwa kwenye Mto Thames kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 350 tangu kutoka kwa mkasa wa Moto Mkubwa.

Mfano huo ulikuwa na umbali wa mita 120.

Wakati wa mkasa huo wa moto ulioendelea kwa siku nne, nyumba 13,000 ziliteketea, yakiwemo majengo muhimu kama vile kanisa la St Paul's Cathedral.