Wanachama wa ANC waandamana dhidi ya rais Zuma

Waandamana dhidi ya uongozi wa rais Jacob Zuma
Image caption Waandamana dhidi ya uongozi wa rais Jacob Zuma

Kundi moja la wanachama wa ANC nchini Afrika Kusini linapinga uongozi dhidi ya Jacob Zuma.

Wanayaita maandamano hayo #OccupyLuthuliHouse,wakitaja makao makuu ya chama hicho mjini Johannesburg,mji mkuu wa taifa hilo.

Lakini waandamanaji wamepunguza kasi ya maandamano yao baada ya usalama kuimarishwa.

Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko ambaye yuko katika eneo la maandamano hayo anasema kuwa yanaendelea kuwa mabaya.

Ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema wanajeshi wa zamani kwa jina uMkhonto we Sizwe,wanazuia waandamanaji kuingia katika afisi ya katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe.

Lakini wanajeshi hao wa zamani wamekuwa wakitumia nguvu.