Kwa nini betri za Lithium hulipuka?

Uamuzi wa kampuni ya simu ya Samsung wa kusitisha mauzo ya simu mpya ya Galaxy Note 7 kutokana na ripoti za kulipuka kwa betri zake ni hatua isiyokuwa ya kawaida kwaa kampuni kubwa ya kiteknolojia.

Simu zinazowekwa chaji
Image caption Simu zinazowekwa chaji

Kampuni hiyo imesema kuwa imebaini kasoro iliopo katika betri hizo lakini haikutoa maelezo zaidi.

Lakini iwapo Betri ya Lithium-ion inashika chaji haraka ni hatari sana kunapotokea kasoro kwa sababu huenda ikasababisha moto.

Mtaalam mmoja ameiambia kampuni hiyo kutafuta madini mbadala ya lithium.

''Nadhani tunafaa kuwa na wasiwasi na kutafuta betri zilizo salama ,''alisema mtaalam wa kuhifadhi nishati Profesa Clare Grey kutoka chuo kikuu cha Cambridge.

''Hilo ni lengo zuri la utafiti na maendeleo viwandani''.

Hatahivyo Profesa Grey anasema kuwa watu hawafai kuwa na hofu.

Kumekuwa na visa 35 vya Galaxy Note 7 kushika moto duniani baada ya mauzo ya takriban simu milioni 2.5,kulingana na Samsung.

Betri za Lithium zinazotumika na Samsung hutumika sana katika viwanda vya kiteknolojia-Lakini ni nini inachozifanya kuwa hatari?.

Ni muhimu kujua vile zinavyofanya kazi.Betri hizo huwa na Cathode,Anode na Lithium.

Image caption Simu yenye bteri iliolipuka

Cathode na Anode huwa zimetawanywa na maji maji yanayoitwa Elektrolait pamoja na kifaa kilicho na mashimo madogo madogo kwa jina kitawanyishi.

Lithium hupitia kitawanyishi hicho ndani ya majimaji hayo.

Iwapo Betri inapata chaji haraka ,na kupata joto,Lithium huzunguka katika Anode ambayo husababisha moto.

Kwa kawaida kuna eneo linalodhibiti chaji inayoingia katika betri hiyo,alisema Profesa Grey.

Betri huwekewa muda ili zisiweze kupata chaji kwa haraka.Hii ndio maana huchukua mda mrefu mtu anapochaji betri.

Lakini betri huanza kutoa ishara za kufura kabla ya kufeli kabisa kwa sababu seli zilizo ndani yake hufura na kupasuka lakini kufura huko hakutokei mara kwa mara.

Na iwapo haitafura utahisi joto lisilo la kawaida katika simu,lakini ukweli ni kwamba simu zetu huongeza joto wakati zinapotumika .

Hatahivyo kampuni hiyo inasema kuwa unapohisi betri yako imeanza kuwa na joto itoe na ununue nyengine.