Utafiti: wanawake huomba nyongeza ya malipo bila mafanikio

Mwanamke aliye ajiriwa Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption 25% ya wanaume walikua na uwezekano zaidi wa kupata nyongeza ya mshahara walipoulizwa, ulibaini utafiti

Dhana kwamba wanawake hupata malipo kidogo kuliko wanaume kwasababu hawashinikizi ipasavyo suala hilo katika maeneo yao ya kazi si kweli ,utafiti mpya umebaini.

Wanawake wana uwezo sawa na wanaume wa kuomba nyongeza ya mshahara - lakini kile kinachobainika ni kwamba wana uwezekano mdogo wa kupata malipo, kulingana na utafiti.

Uchunguzi uliofanywa na chuo cha mafunzo ya kibiashara cha Cass, chuo kikuu cha Warwick pamoja na kile cha Wisconsin, uliwaangazia wafanyakazi 4,600.

Ulibaini kuwa "hakuna ushahidi wa dhana ya mienendo ya "usiri wa wanawake'', ambapo wanawake walijiepusha na kuomba nyongeza ya malipo ya pesa.

Kwa mara ya kwanza, uchunguzi uliengua athari yoyote kutoka kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za muda ambao hupata malipo ya chini kuliko wenzao wanaofanya kazi katika muda kamili, kwa kulinganisha malipo ya wanaume wanaofanya kazi muda kamili na wanawake wanaofanya kazi muda kamili wa kazi, wanaume wanaofanya kazi za muda na wanawake wanaofanya kazi za muda.

Walipolinganisha wanaume na wanawake wanaofanya kazi zinazofanana, 25% ya wanaume walikua na uwezekano zaidi wa kupata nyongeza ya mshahara walipoulizwa, ulibaini uchunguzi huo.

Utafiti pia ulidhihirisha kuwa hakuna ushahidi wowote kwa dhana kwamba wanawake walikuwa wanasitasita kuomba nyongeza ya mshahara kwasababu walikuwa na hofu zaidi ya kuwakera wakuu wao wa kazi , ama kwasababu ya kuepuka ubaguzi dhidi ya wanawake.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Msingi wa utafiti huo ni taarifa kutoka uchunguzi wa Australia wa 2013 - 14 kuhusu mahusiano katika maeneo ya kazi.

Walipokuwa wakitathmini matokeo hayo, watafiti hao walizingatia idadi ya waajiri na viwanda, ikiwa wafanyakakazi walikuwa ni wazazi, pamoja na uwezo wao wa kikazi.

Msingi wa utafiti huo ni taarifa kutoka uchunguzi wa Australia wa 2013 - 14 kuhusu mahusiano katika maeneo ya kazi.

Australia inadhaniwa kuwa ni nchi pekee yenye mfumo sahihi wa kuweka taarifa zinazoonesha kama waajiriwa waliwahi kuomba nyongeza ya malipo, na kwa nini walifanya hivyo ama kwanini hawajawahi kufanya hivyo.

Andrew Oswald, profesa katika masuala ya uchumi na sayansi ya tabia katika Chuo kikuu cha Warwick, anasema alishangazwa na matokeo ya utafiti huo.

" Ukweli ni kwamba wanawake hawaombi nyongeza ya malipo mara kwa mara kama wanaume ndio dhana maarufu''.Ni kitu cha kawaida kwa wanawake kukisema na kuamini, lakini ushahidi wote unaonyesha majibu tofauti ya vile inavyosemwa na kuaminiwa, kwa hiyo ni vigumu sana kulipima kikamilifu suala hili kisayansi."

Alisema uwezekano mmoja ni kwamba huenda wanaume wanaoomba nyongeza ya malipo bila mafanikio, walitunza siri hiyo, huku wanawake " wakiwa wazi na kuwaeleza marafiki zao kuhusu hilo".

Utafiti huo pia ulibaini kuwepo kwa utofauti huo kulingana na umri, wanawake na wanaume walio chini ya miaka 40 ambao waliomba ama kupokea nyongeza ya mshahara kwa kiwango sawa, ambapo watafiti waliweza kusema mienendo yao ya kuomba nyongeza ya mshahara ilianza kubadilika.