Je,wajua Vitamin D hupunguza pumu?

Matumizi ya virutubisho vya vitamin D pamoja na dawa za pumu hupunguza hatari ya shambulio la ugonjwa wa pumu.
Image caption Matumizi ya virutubisho vya vitamin D pamoja na dawa za pumu hupunguza hatari ya shambulio la ugonjwa wa pumu.

Matumizi ya virutubisho vya vitamin D pamoja na dawa za pumu hupunguza hatari ya shambulio la ugonjwa wa pumu.

Utafiti uliofanywa na watafiti wa Cochrane umebaini kwamba vinapunguza shambulio la wagonjwa wanaotumia steroids.

Lakini watafiti wanasema kuwa haijulikani iwapo inawasaidia wagonjwa walio na upungufu wa Vitamin D.

Wanasema utafiti zaidi unahitajika kabla ya kuwapa wagonjwa ushauri rasmi.

Walipendekeza kuzungumza na wauza dawa ili kupata ushauri kabla ya kutumia virutubishi vya Vitamin D.

Kiongozi wa watafiti hao Profesa Adrian Martineau anasema kuwa walibaini kwamba Vitamin D inapunguza makali ya ugonjwa wa Asthma,bila kusababisha athari zozote.