China yaonya kuhusu uhuru wa Hong Kong

Wanaharakati wanaotetea uhuru wa Hong Kong waonywa na Uchina
Maelezo ya picha,

Wanaharakati wanaotetea uhuru wa Hong Kong waonywa na Uchina

China imesema kwamba inaunga mkono hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayetetea uhuru wa eneo la Hong Kong.

Onyo hili limejiri baada ya wanaharakati wanaounga mkono uhuru wa Hong Kong kushinda uchaguzi wa bunge.

Msemaji wa afisi ya China inayohusika na masuala ya Hong Kong na Macao amesema Beijing inapinga harakati zote za kutetea uhuru wa Hong Kong ndani na nje ya bunge

Raia wengi wa Hong Kong wameghadhabishwa na kile wanasema kuwa juhudi za China kuzima haki na uhuru wa kimsingi.