Mwanamke mwenye asili ya Kihindi ashinda taji la malkia wa Urembo Japan

Mshindi wa taji la malkia wa urembo nchini Japan Priyanka Yoshikawa
Image caption Mshindi wa taji la malkia wa urembo nchini Japan Priyanka Yoshikawa

Mwanamke mwenye asili ya Kihindi ameshinda taji la malkia wa Urembo nchini Japan,ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa mtu mwenye asili ya makabila mawili kushinda taji hilo.

Priyanka Yoshikawa mwenye umri wa miaka 22 amesema kuwa atatumia ushindi wake kubadili mafikira ya watu.

Mwaka uliopita mshindi wa taji hilo Miss Ariana Miyamoto alikuwa wa kwanza mwenye asili yenye makabila mawili.

Wakosoaji wanalamika kwamba raia mwenye asili ya Japan angefaa kushinda.

Image caption Ariana Miyamoto alishinda taji hilo mwaka 2015

Ni asilimia 2 ya watoto waliozaliwa nchini Japan ambao huwa wana asili mbili ama haafua kama wanavyowaita raia wa Japan.

''Sisi sote ni raia wa Japan'', alisema bi Yoshikawa .''Ndio babangu ni Muhindi na najivunia hilo,ninafurahi kwamba nina Uhindi ndani yangu,lakini hilo halimaanishi kwamba mimi sio Mjapan''.