Muhubiri mwenye itikadi kali afungwa miaka 5

Choudary
Image caption Choudary

Muhubiri mwenye itikadi kali Anjem Choudary nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na nusu kwa kuitisha usaidizi kutoka kwa kundi la Islamic State.

Choudary mwenye umri wa miaka 49 alihukumiwa katika mahakama ya Old Bailey baada ya kuliunga mkono kundi hilo mtandaoni.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa wafuasi wa Choudary walitekeleza mashambulio nchini Uingereza na ugenini.