Aliyefanyiwa upandikizaji wa kwanza wa uso afariki

Isabelle Dinoire ambaye alifanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikiza wa sura amefariki
Maelezo ya picha,

Isabelle Dinoire ambaye alifanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikiza wa sura amefariki

Madaktari nchini Ufaransa wamefichua kwamba mwanamke aliyefanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikizaji wa sura alifariki mapema mwaka huu.

Hospitali moja imesema kuwa Isabelle Dinoire alifariki baada ya matatizo yanayohusishwa na upasuaji huo .

Alifanyiwa upasuaji huo uliochukua saa 15 mwaka 2005 baada ya kujeruhiwa na mbwa.

Madaktari waliutengeza mdomo wake,pua na taya katika upasuaji huo wa kwanza kuwahi kufanyika.

Hospitali hiyo imesema kuwa kifo chake hakikutangazwa hadi sasa ili kulinda faragha ya familia yake.

Alikuwa na umri wa miaka 49.