Niger imepiga marufuku mauzo ya nje ya punda

Punda aliyebeba kuni Haki miliki ya picha AFP
Image caption Niger: Mwaka 2015 punda 27,000 waliuzwa nje ya nchi na hadi kufikia mwaka huu punda, 80,000 wamekwisha uzwa nje

Taifa la Niger limepiga marufuku mauzo ya nje ya punda baada ya serikali kuhofia kwamba idadi ya wanayama hao inapungua.

Serikali inasema wannyama hao wanaendelea kutoweka kwasababu wanauzwa kwa wingi nje ya nchi hususan katika mataifa ya bara Asia.

Nchini Niger, punda hutumiwa kwa shughuli za usafirishaji.

Takwimu zinaonyesha kuwa mnamo mwaka 2015 punda 27,000 waliuzwa nje ya nchi na hadi kufikia mwaka huu punda, 80,000 wamekwisha uzwa nje.

Uchina ni muagizaji mkuu wa ngozi za punda kwa ajili ya kutengenezea madawa ya kienyeji.

Hivi karibuni, Burkina Faso ilipiga marufuku mauzo ya nje ya mizoga ya punda.