Kofi Annan aonywa asiingilie masuala ya Myanmar

Kofi Annan
Image caption Wanaompinga Kofi Annan Mynmar wanasema kwamba hapaswi kuingilia mzozo wa ndani ya nchi

Mamia ya wanaharakati wa Kibudha nchini Myanmar wamemzomea katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, alipowasili katika jimbo la Rakhine.

Bw Annan aliombwa na kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, kuongoza tume itakayochunguza mzozo wa kijamii katika jimbo hilo lililoko magharibi mwa nchi.

Wanaompinga wanasema suala hilo ni suala la ndani ya nchi na kwamba wageni hawapasi kuingilia masuala yao.

Maelfu kwa maelfu ya jamii ya dhehebu la Waislam wa Rohingya wamesambaratika kutokana na mashambulio ya mabudha walio wengi. Wengi wamekimbia nchi.

Ghasia hizo zimesababisha baadhi kuhoji juhudi za Aung San Suu Kyi za haki za kibinadamu nchini hum