Mahakama ya Afrika kusini yaagiza watoto wa wageni wapewe uraia

Ramani ya Afrika kusini
Image caption Uamuzi wa mahakama utakuwa na adhari kubwa kwa maelfu ya watoto wakiwemo wale ambao wamewekwa kwenye orodha ya kuasiliwa.

Mahakama ya rufaa nchini Afrika kusini imetoa uamuzi imetoa uamuzi utakaoidhinisha uraia wa watoto wanaozaliwa katika nchi hiyo ambao wazazi wao ni raia wa kigeni.

Uamuzi huo unafuatia kesi iliyodumu kwa muda wa miaka miwili, kuhusu watoto ambao hawakuwa na uraia na ambao hawakuwa na fursa ya kupata elimu, huduma za afya na za kijamii nchini Afrika Kusini.

Kesi hiyo ilimuhusisha msichana mmoja mwenye umri wa miaka minane ambaye wazazi wake ni raia wa cuba waliokuwa wakiishi nchini nchini humo.

Mahakama hiyo ya rufaa imeagiza kuwa msichana huyo sasa aweza kuwa raia wa taifa alilozaliwa.

Aidha mahakama hiyo imeagiza wizara ya mambo ya ndani kuweka mikakati ya kuwasaidia watoto wengine ambao wanaojikuta bila uraia kwa sababu Kama hiyo , kupewa uraia nchini Afrika Kusini.

Uamuzi huo sasa utakuwa na adhari kubwa kwa maelfu ya watoto wakiwemo wale ambao wamewekwa kwenye orodha ya kuasiliwa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Afrika Kusini amesema wizara yake imeafiki uamuzi huo, ila itachunguza kila kesi kuambatana na hali yao halisi kabla ya kutoa uraia.