Apple yatarajiwa kuzindua iPhone 7

Apple iphone Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kutakuwa na mabadiliko?

Apple inatarajiwa kuzindua simu mpya zaidi ya iPhone Jumatano, wengi wakitarajia kuona ikiwa simu hiyo mpya itaendelea kutumia kifaa ya kusikizia sauti, yaani headphone jack.

Uzinduzi huo unafanyika siku chache baada ya mshindani mkubwa wa kampuni hiyo Samsung kulazimika kusitisha uuzaji wa simu yake ya kisasa zaidi ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri.

Wachanganuzi wa masuala ya teknolojia wanaendelea kujadiliana kuhusu sifa na vifaa vipya ambavyo huenda vikazinduliwa kwenye simu hiyo mpya.

Wengi wanatarajia Apple itupilie mbali tundu la kuwekwa headphone jack, na badala yake kuwe na tundu moja pekee.

Hili litawafanya wanaotumia simu hizo kutumia headphone za teknolojia ya Bluetooth au zile zinazoweza kutumia tundu la Lightning la vifaa vya Apple ambalo pia hutumiwa kuweka chaji.

Hata hivyo, vifaa vya awali havitaacha kutumika kabisa, na Apple inatarajiwa kuzindua kifaa ambacho kitamuwezesha mtu kukitumia uunganisha headphone na simu na kuendelea kuitumia.

Baadhi ya ammbo mapya yaliyozinduliwa karibuni zaidi kwenye iPhone yamekosa kuvutia watu sana.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simu hiyo inatarajiwa kufuata mtindo wa iPhone kwa kuwa na ukubwa mara mbili

Na wengi wanatarajia hilo lifanyike baada ya uzinduzi Jumatano mjini San Francisco, California.

Uwezo wa kamera hata hivyo unatarajiwa kuimarishwa zaidi. Huenda simu hizo zikawa na lens mbili za kamera ambazo zitamuwezesha mtu kupiga picha za ubora wa hali ya juu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii