Wakonta Kapunda, binti aliyeandika kwa ulimi, apata kifaa

Wakonta Kapunda

Unamkumbuka Wakonta Kapunda? Binti Mtanzania mwandishi wa miswada ya filamu anayeandika kwa kutumia ulimi wake?

Wakonta alipata ajali siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita. Ajali hiyo ilimuacha akiwa amepooza kwanzia shingoni kushuka chini na kumfanya kutoweza kutumia mkono yake kuandika.

Wiki kadhaa zilizopita, BBC iliporusha habari yake Msamaria Mwema mmoja aliguswa kumsaidia

Kupitia kipindi cha televisheni cha Focus on Africa katika BBC World Service, mwanadada Olivia Soko kutoka Afrika ya Kusini aliguswa kufanya kitu kumsaidia Wakonta.

Huwezi kusikiliza tena
Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi

Akiwa mkurugenzi wa kampuni ya Whirlmarket Technologies, Olivia alijitolea kutoa msaada wa programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking.

Jinsi Program hii inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji yeye anazungumza anachotaka kukiandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji

Wakonta alijaribu kuitumia jana, akaifurahia, lakini bila shaka atahitaji muda zaidi ili aizoee vizuri.

Familia yake pia imefurahishwa sana na msaada huu.