Trump aungwa mkono na wanajeshi 88 waliostaafu

Donald Trump
Image caption Donald Trump

Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ameungwa mkono na viongozi 88 wa zamani wa jeshi katika barua ya wazi kulingana na kampeni yake.

Kundi hilo lenye majenerali wastaafu pamoja na admirali waliamua kuwa kiongozi huyo ana uwezo wa kuwa kamanda mkuu wa jeshi.

Bwana Trump ambaye ameangazia maswala ya wazee wakati wa kampeni yake alitaja uungwaji mkono huo kuwa heshima kubwa.

Hatahivyo amepinga madai ya utumizi mbaya kuhusu ufadhili wa kisiasa kwa afisa mmoja wa Florida.

Gazeti la The Washington liliripoti siku ya Jumatatu kwamba mwaka 2013,mwanasheria mkuu wa Florida Pam Bondi alipendekeza mashtaka ya udanganyifu dhidi ya chuo kikuu cha Trump.

Lakini alisitisha uchunguzi huo baada ya mchango wa dola 25,000 kutolewa na wakfu wa Donald Trump kusaidia kampeni yake ya kisiasa.

Bwana Trump alipigwa faini kwa kuwa hakutangaza mchango wake kwa halmashauri ya ushuru nchini Marekani.