Taylor swift awachana na mpenziwe

Tom Hiddleston na Swift Taylor
Image caption Tom Hiddleston na Swift Taylor

Taylor Swift na Tom Hiddleston wameachana baada ya kuwa na uhusiano wa miezi mitatu kulingana na ripoti kadhaa nchini Marekani.

Uvumi ulianza kwamba wapenzi hao waliopewa jina la utani ''Hiddleswift'' walikuwa pamoja baada ya kuonekana wakitaniana katika tamasha la Met Gala mnamo mwezi Mei.

Tangu wakati huo,wamekuwa pamoja wakionekana pamoja katika kila pembe ya dunia ikiwemo ziara ya Uingereza kuonana na familia ya Tom.

Lakini imeripotiwa kwamba wameshindwa kuendeleza penzi lao.

Hakuna tamko lolote rasmi kutoka kwa Tom ama Taylor kufikia sasa lakini duru zinazowajua wapenzi hao zimeongezea: ''huwa pamoja kila mara na watasalia kuwa marifiki wakubwa lakini hawaoni kwamba urafiki huo unawezekana kimapenzi''.