Uturuki na Marekani kushambulia ngome ya IS Syria

Wapiganaji wa islamic State waliopo mjini Raqqa nchini Syria
Image caption Wapiganaji wa islamic State waliopo mjini Raqqa nchini Syria

Uturuki imekariri mpango wa Marekani kushirikiana nayo kufanya oparesheni ya pamoja kuwafurusha wanamgambo wa Islamic State kutoka mji wa Raqqa ambao ni ngome kuu ya wapiganaji hao nchini Syria.

Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema mazungumzo baina yake na Obama juu ya suala hilo,yanaendelea na kwamba taifa lake liko tayari kushirikiana naye.

Majeshi ya Uturuki yamekuwa yakiendeleza oparesheni kali Kaskazini mwa Syria dhidi ya waasi wa kikurdi.