Simu mpya ya Apple iPhone 7 isiyo na headphone za kawaida

iPhone 7 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Afisa mkuu mtendaji wa Apple Tim Cook alizindua iPhone 7 katika jimbo la California

Kampuni ya Apple imethibitisha kwamba simu yake mpya ya iPhone haitakuwa na tundu la kawaida la kifaa cha kusikiza sauti, ambacho kwa Kiingereza hufahamika kama headphone.

Simu hiyo ya iPhone 7 badala yake itatumia teknolojia ya Apple ya lightning, ambayo itawezesha mtu kutumia tundu moja kuunganisha simu na vifaa vingine.

Apple pia watavumisha kutumiwa kwa visikizia sauti ambavyo havitumii nyaya, na imetoa aina yake ya earphone zinazojulikana kama Airpods.

Kampuni hiyo imesema imehitaji kutumia ujasiri kuchukua hatua hiyo.

Hata hivyo, hatua hiyo huenda ikawaudhi baadhi ya wateja ambao sasa watahitajika kununua kifaa unganishi yaani adapter ndipo waweze kutumia visikizia sauti.

Kampuni hiyo ya Marekani ilizindua simu hiyo yake mpya katika hafla mjini San Francisco, Marekani.

Hii imejiri baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kushuka kwa mauzo ya simu za iPhone na kupungua kwa sehemu inayodhibitiwa na kampuni hiyo sokoni.

Sifa nyingine:

  • kitufe cha nyumbani sasa kinaweza kutofautisha uzito kinapobonyezwa na kutoa mtikisiko. Kitufo hicho sasa hakiingii ndani ya simu.
  • simu hizo zinaweza kuingizwa ndani ya maji ya kina cha 1m (3.2ft) kwa dakika 30 wakati mmoja bila kuharibika
  • aina kubwa ya iPhone 7 Plus ina lensi mbili za kamera sehemu ya nyuma, ambayo inaimarisha uwezo wa kupiga picha.

Uzinduzi wa simu hizo umetokea siku chache baada ya Tume ya Ulaya kuamua Apple inafaa kulipa €13bn (£11bn) kama malimbikizi ya kodi kwa Ireland, uamuzi ambao Apple imekata rufaa.

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Kitufe cha nyumbani cha iPhone 7 kitatikisika kufikisha ujumbe kwa anayetumia

Airpod

Kisikizia sauti cha 3.5mm kilivumishwa sana na vicheza muziki vya Walkman vya kampuni ya Sony, lakini kilitumiwa mara ya kwanza katika redio zilizotengenezewa Japan mwaka 1964.

Apple imedokeza mara nyingi nia yake ya kutaka kuacha kutumia viunganishi na vifaa vingine vya zamani kabla ya wapinzani wake.

Lakini wakati huu hawakutangulia.

Moto Z ya Lenovo na vifaa vingine vya LeEco, ya Uchina vilizinduliwa bila tundu la kisikizia muziki hicho cha 3.5mm mapema mwaka huu.

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Apple imesema kuondoa tundu hilo la headphone ya 3.5mm kutanusuru nafasi inayoweza kutumiwa kuongeza vitu vingine

Airpods zitagharimu takriban £159.

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Airpods zina kifaa cha kuhifadhia ambacho kinaweza kuongeza chaji

Airpods pia zina uwezo wa kugundua zinapoingizwa masikioni. Hii inaziwezesha kusitisha uchezaji muziki zinapochomolewa masikioni.

Unaweza pia kuzielekeza kwa kutumia programu ya Siri. Hata hivyo, lazima ziwekwe chaji kivyake ingawa Apple inasema zinaweza kukaa na chaji kwa hadi saa tano. Kifaa chake cha kuhifadhia kinawezesha mtu kutumia kwa hadi saa 24.

Kampuni Mauzo Mabadiliko mwaka hadi mwingine Sehemu ya soko kufikia Juni 2016
Julai 2015 - Juni 2016
Samsung 323.3 milioni +4.3% 23%
Apple 214.4 milioni -3.6% 12%
Huawei 120.3 milioni +38.2% 9%
Oppo 68.2 milioni +91.3% 7%
Vivo 53.7 milioni +68.4% 5%
Lenovo 61.0 milioni -28.5% 3%
Xiaomi 60.5 milioni -10.6% 4%
LG 57.6 milioni -6.9% 4%
Chanzo: IDC

Kamera mbili

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Kuwa na lensi mbili kunawezesha iPhone 7 Plus kuleta karibu zaidi kitu kinachopigwa picha

Bei ya iPhone 7 itakuwa kuanzia £599 hadi £799, kwa kutegemea uwezo wake wa kuhifadhi data. Kwa iPhone 7 Plus ni kuanzia £719 hadi £919.

Bei ya kwanza sokoni kwa iPhone 6S ilikuwa £539 na iPhone 6S Plus ilikuwa £619, ingawa uwezo wake wa kuhifadhi data ulikuwa chini.

Simu hizo zitaanza kuuzwa tarehe 16 Septemba.

Teknolojia zilizotupwa

Apple imekuwa na tabia ya kuacha mapema teknolojia inazodhani zimepitwa na wakati.

Miongoni mwake ni:

  • Floppy disk drive (1998)
  • Dial-up modem (2005)
  • CD/DVD drive (2008)
  • 30-pin connector (2012)
  • USB 3 ports (2015)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii