UN yawasaidia wapiganaji wa Machar DR Congo

Dkt Machar hajaonekana hadharani tangu akimbie mapigano Juba Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dkt Machar hajaonekana hadharani tangu akimbie mapigano Juba mwezi Julai

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema wamesaidia kuwasafirisha zaidi ya wapiganaji 100 kutoka Sudan Kusini hadi vituo vya afya nchini DRC kupokea matibabu.

Msemaji wa UN Stephane Dujarric amesema wapiganaji hao, watiifu kwa kiongozi wa waasi Riek Machar, walikuwa katika hali mbaya kiafya walipowasili nchini humo.

Bw Machar mwenyewe alipewa usaidizi wa kimatibabu na wanajeshi wa UN baada ya kujeruhiwa mwezi uliopita katika mapigano nchini Sudan Kusini.

Baadaye aliondoka DRC na kuelekea Sudan. Alitibiwa kwa muda na kuruhusiwa kuondoka hospitalini mwishoni mwa mwezi Agosti ingawa bado amesalia nchini Sudan.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii