Kidum ajipata njia panda nchini Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Kidum ajipata njia panda nchini Burundi

Mwanamuziki mashuhuri wa Burundi mwenye makazi yake nchini Kenya Nimbona Jean Pierre almaarufu Kidum amejikuta matatani akiwa nchini mwake Burundi baada ya kulaumiwa na wapinzani kuwa amekwenda huko kuupigia debe utawala wa Rais Pierre Nkurunziza.

Rasmi, Kidum yuko Burundi kutumbuiza kwenye tamasha ya biashara ilioandaliwa na Ubalozi wa Kenya nchini Burundi.

Lawama dhidi yake zimekuwa nyingi baada ya Kidum kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, kiasi ya kupata vitisho huku ulinzi wake ukiimarishwa.

Mwandishi wetu wa Bujumbura, Ramadhani Kibuga amezungumza na Kidum kuhusu tuhuma hizo.