Kenya yashinda dhahabu Olmpiki za walemavu Rio

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Samwel Kimani wa Kenya ameongoza kifuatiwa na Odair Santos wa Brazil alishinda medali ya fedha, huku Erick Sangwa Kenya akishinda medali ya shaba

Mwanariadha wa Kenya Samwel Kimani amejishindia medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olympiki ya walemavu, Paralympiki 2016, baada ya kushinda mbio za 5000m kwa wanaume wasioona.

Odair Santos wa Brazil alishinda medali ya fedha, huku Erick Sangwa Kenya akishinda medali ya shaba.

Licha ya kwamba Waingereza wengi wamefanya vizuri tayari, lakini kwa Lorraine Lambert na mshirika wake katika mchezo wa kulenga shabaha Karen Butler wameshindwa kufuzu kwa fainali za wanawake mita 10 kulenga shabaha.

Kenya ilishinda medali mbili za dhahabu katika Olympiki ya walemavu ya mwaka 2012 mjini London na medali 6 kwa ujumla.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muingereza Lorraine Lambert (pichani) ameshindwa kufuzu kwa fainali za kulenga shabaha mita 10 upande wa wanawake

Wanariadha kutoka maeneo mbali mbali duniani watakuwa wakishindania 38 zilizopo katika siku ya kwanza ya michezo hii.

Matukio mengine ni pamoja na kulenga shabaha, riadhana judo.

Michezo ya Olyimpiki ya walemavu- Paralympics imegubikwa na matatizo, ikiwemo upungufu wa pesa za udhamini, mauzo hafifu ya tiketi za michezo, na kupigwa marufuku kwa Urusi kushiriki kutokana na taifa hilo kudhamini matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.