Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wa Muungano wa Ulaya wamekutana kujadili mkataba wa kibiashara
Huwezi kusikiliza tena

Viongozi wa Afrika Mashariki na Muungano wa Ulaya wamejipa miezi mitatu kabla ya kusaini makubaliano

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeongeza miezi mitatu zaidi kuweza kusaini makubaliano ya kiuchumi kati ya Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Ulaya kuweza kupata muda zaidi wa kuyapitia tena. Rais wa Tanzania John Magufuli amebainisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeiomba EU kutoiadhibu Kenya kwa kuchelewa kusaini mkataba huo

Tanzania na Uganda zimekuwa zikipinga mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)