Sababu ya Tanzania kupinga mkataba wa EU
Huwezi kusikiliza tena

Sababu ya Tanzania kupinga mkataba wa EU

Tanzania na Uganda zimekuwa zikipinga mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao kwa kifupi unafahamika kama EPA.

Mashauriano kuhusu mkataba huo yameendelea kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Mkataba huo ni miongoni mwa mambo yanayozungumziwa katika mkutano wa dharura wa wakuu wa EAC.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga ambaye anafafanua sababu za Tanzania kuupinga mkataba huo.