Israel kudhibiti mipaka yake,ardhini.

Syria
Image caption Syria kudhibiti mipaka yake

Israel imeanza kujenga kizuizi cha chini ya ardhi ambacho kitanyoosha mipaka yake yote na Gaza. Maofisa wa Israel wamesema kuwa kizuizi hicho kinalenga kuzuia vikosi vya kipalestina kuchimba mashimo ambayo huwasaidia kutekeleza mashambulizi Israel, kama ilivyokuwa hapo nyuma.

Tayari Gaza imezungukwa na ukuta wa ngome na minara, nyaya na kamera ili kuthibiti ulinzi zaidi. Ambapo ujenzi wake unatazamiwa kukamilika baada ya mwaka mmoja.

wakati huo huo

Zaidi ya mashirika 70 ya kibinadamu ya nchini Syria yanawatuhumu mawakala wa misaada wa Umoja wa Mataifa kwa kuruhusiwa kijanja kutumiwa na serikali ya Rais Bashar al-Assad. Mashirika ya kisyria yametoa mfano mmoja kuwa kushindwa kwa Umoja wa Mataifa kumaliza kuzingirwa kwa maeneo ambayo uasi umefanyika.

Makundi hayo yanataka uchunguzi ufanyike kuhusu ushawishi wa serikali juu ya Damascus kulingana na mtandao wa kibinadamu wa Umoja wa mataifa. Ambapo wanasema mpaka sasa na madai mengine yakutaka kukomesha ubadilishanaji wa taarifa kwa mawakala wake.