Kwa Picha: Afrika wiki hii 2-8 Septemba 2016

Mkusanyiko wa picha kutoka Afrika na za Waafrika kwengineko wiki hii:

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoto waliotoroka makwao baada ya vita kuzuka eneo la Darfur, Sudan, washiriki katika mchezo wa Pool siku ya Jumanne...
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katika kambi iyo hiyo, siku ya Jumanne, watoto wakusanyika kununua aiskrimu...
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Salamu za kikwetu! Mchezaji wa timu ya Africa Kusini ya walemavu amchangamkia mwenzake kwa salamu za aina yake katika sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki kwa walemavu mjini Rio, Brazil siku ya Jumatano.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Subira huvuta kheri! Siku iyo hiyo, kijana aonekana akisubiri kwa hamu kuwasili kwa shujaa wa michezo ya Olimpiki katika uwanja wa ndege wa Johannesburg kutoka Rio.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Karibu nyumbani! Wayde van Niekerk, aliyeshinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 400 awasili Afrika kusini - Alivunja rekodi ya dunia.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgeni njoo mwenyeji apone! Rais wa Nigeria aonekana kufurahishwa na zawadi aliokabidhiwa na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg mjini Abuja Ijumaa. Kulingana na msaidizi wa rais, zawadi hiyo ni mfano wa ndege isiyokuwa na rubani, itakayorahisisha upatikanaji wa huduma za mitandaoni barani Afrika.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku iliyofuata, akina dada nchini Nigeria wacheza ngoma za kuipa motisha timu ya taifa ya soka, Super Eagles, ambapo waliinyuka Tanzania bao 1 kwa 0. Hata baada ya ushindi huo, Nigeria ilikosa nafasi katika dimba la fainali ya mataifa bingwa barani Afrika litakaloandaliwa mwaka ujao.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wasichana watembea katika mtaa Maiduguri, jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria, Bono. Picha hii ilitolewa siku ya Jumatano.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Picha hii ni miongoni mwa picha maalum za shirika la habari la Reuters, kuhusu uharibifu uliosababishwa na vita vya Boko Haram. Huu ni msikiti uliojawa na matundu ya risasi katika eneo la Bama.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alhamisi, mfanyikazi nchini Ivory Coast akitembea karibu na daraja ya reli inayoelekea Burkina Faso, iliyoharibiwa karibu na mto wa Nzi. Itachukua miezi kadhaa kabla ya shughuli za kawaida kuendelea kwenye reli hiyo.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aamkaye mapema ajua riziki! Kusini mwa Ivory Coast, mvuvi aanza siku yake jua likichomoza, mjini Abidjan, siku ya Ijumaa.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanasema starehe ya mbwa kukalia mkia...! Raia wa Libya wabarizi ufuoni katika mji wa mwambao, Benghazi siku ya Jumanne.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakristo waimba kanisani siku ya Jumapili, mjini Libreville, Gabon, katika kanisa la mchungaji Georges Bruno Ngoussi, mmiliki wa vituo vya radio na runinga vilivyovamiwa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi.
Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtu mume ni kazi! Siku ya Jumanne, mwanamme nchini Zimbabwe ajizatiti kuosha ukuta uliochafuliwa kwa maandishi ya kuikosoa serikali, mjini Harare.