Mtindo wa kupanda maua kwenye viatu Kenya

Image caption Upandani wa mimea ya maua kwenye viatu vikuu

Mjasiriamali raia wa Kenya Wanjiru Waweru-Waithaka ameamua kupanda mimea ya maua katika viatu vya plastiki vikuu kuu.

Image caption Mimea hii ya maua iliyopandwa kwenye viatu vya plastiki huwavutia wateja wa Bi Wanjiru Waweru-Waithaka

Mwandishi wa BBC Taurai Munda alipiga picha hizi alipozuru Kenya.

Anasema mimea ya maua inayopandwa kwenye viatu vya plastiki vikuu huwafanya wateja wanaotembelea biashara yake ya kuuza vitanda vya watoto, katika mji wa Kikuyu nje ya jiji la Nairobi watabasamu.

Image caption Mjasiliamali wa Kenya Wanjiru Waweru-Waithaka huuza vitanda vya watoto