Hillary: Ipo tofauti ya Rusha Roho na Taarab
Huwezi kusikiliza tena

Patricia Hillary: Kuna tofauti kati ya Rusha Roho na Taarab

Mahadhi ya muziki wa taarab asilia kwa miaka mingi umekuwa maarufu katika pwani ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo muziki huo unadaiwa kupoteza umaarufu wake kutokana na kuingia kwa mfumo mpya wa twaarabu al-maarufu kama rusha roho.

Baadhi ya wanamuziki wa zamani bado msimamo wao upo pale pale kwamba ya kale ni dhahabu.

Mwandishi wa BBC Munira Hussein amezungumza na Patricia Hillary, nguli wa muziki wa taarab asilia nchini Tanzania.