Mfahamu Ri Chun-hee, mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini

Ri Chun-hee: Haki miliki ya picha Getty Images

Mmwanamke huyu mtangazaji, anayesadikika kuwa na umri wa miaka sabini hivi, amekuwa akipewa jukumu la kutoa matangazo muhimu zaidi ya taifa Korea Kaskazini.

Ndiye hutangaza majaribio ya nyuklia au makombora yakitekelezwa na ni yeye pia hutumiwa kutoa tahadhari kuhusu uovu wa nchi za Magharibi.

Ri Chun-hee amewahi kulia, akacheka na kusema kwa sauti katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini aliyofanya kazi.

Leo, amekuwa tena kwenye runinga kutangaza kutekelezwa kwa jaribio la tano la bomu la nyuklia Korea Kaskazini.

Hakuna anayefahamu umri wake hasa, lakini anadhaniwa kuwa na miaka sabini hivi.

Haya hapa ni mambo tunayoyafahamu kumhusu:

Hupenda rangi ya waridi

Sana vazi lake la Kikorea la chima jeogori, a well-known Korean dress.

Alilivaa akitangaza kutekelezwa ka jaribio la bomu la haidrojeni Januari mwaka huu.

Haki miliki ya picha kctv
Image caption Ri Chun-hee amefanya kazi miaka mingi

Lakini hubadilisha wakati mwingine.

Alivalia mavazi meusi na kuonekana kutekwa na huzuni akitangaza vifo vya viongozi wa Korea Kaskazini.

Image caption Akitangaza kifo cha Kim Jong-il

Huaminiwa sana na watawala

Inaarifiwa kwamba Kim Jong-un humtaka yeye awasilishe binafsi ujumbe wa chama chake kwa ulimwengu.

Ndiye aliyetangaza vifo vya viongozi wa awali: Kim Il-Sung na Kim Jong-Il.

Ri Chun-hee majuzi alitangaza kufanikiwa kwa Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya kuzunguka dunia kwa kutumia roketi. Hilo lilishutumiwa kama njama ya kufanyia majaribio kombora la masafa marefu.

Hubadilisha hisia.

Anaweza kusema kwa sauti na hata kulia akitangaza.

Pia, huzungumza kama mtu mwenye mamlaka akifikisha ujumbe wa viongozi wa Korea Kaskazini.

Huwezi kusikiliza tena
Alipotangaza habari za jaribio la bomu la haidrojeni

Anaonekana kuwa maarufu sana.

Chun-hee huishi Pyongyang, na huonyeshwa runingani akiwa na watu wengi wanaomtazama, kupiga makofi na wakati mwingine kulia.

Huenda asiwe hewani muda mrefu.

Majuzi alsema anataka kuacha kazi ya utangazaji na kuwapa mafunzo watangazaji wengine wa kike wa kutangaza habari za taifa.

Anadaiwa kufurahia maisha.

Chun-hee is anadaiwa kutembelea migahawa bora zaidi na vituo vya burudani Pyongyang.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ri Chun-hee alitangaza vifo vya Kim Jong-Il (Kulia) na babake, Kim Il-Sung (Kushoto)