Moto wa kiwanda wawaua watu 20 Bangladesh

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Moto huo ulisambaa kwa haraka katika nyumba hiyo ya ghorofa nne

Watu ishirini wameuwawa nchini Bangladesh katika moto mkubwa katika kiwanda kimoja, uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji.

Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa viungani mwa mji mkuu Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga ikaongezeka.

Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wazima moto wakiwabeba waathiriwa kwenye ajali hiyo ya moto

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii