Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo

Maelezo ya video,

Mtangazaji wa runinga wa Korea Kaskazini akisoma habari

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kuanza kuweka vikwazo mpya dhidi ya Korea Kaskazini katika kujibu jaribio la silaha za kinyuklia lililotekelezwa na Pyongyang.

Korea kusini inasema itahimiza kuwekwa kwa vikwazo dhabiti ili kuizuia Korea Kaskazini.

Maelezo ya picha,

Korea Kaskazini imefanya majaribio mawili ya nuklia mwaka huu

Serikali za Marekani na korea kusini zimeanza kufanya uchunguzi wa hewa na bahari kuchunguza athari ya vifaa vya mionzi vilivyotumika katika jaribio hilo, na kubaini ni silaha gani iliyofanyiwa majaribio.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana na kutoa taarifa ya kuikosoa vikali majaribio hayo ya Korea Kaskazini.