Kenya yaishawishi Somalia kuondoa marufuku kwa miraa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Karibu ndege 15 zinazosafirisha miraa huwasili mjini Mogadishu kila siku

Kenya inasema kuwa inafanya kila iwezalo kuishawishi serikali ya Somalia kubatilisha uamuzi wa kuzipiga marufuku ndege zinazosafirisha mirraa.

Marufuku hiyo ilitangazwa na Somalia wiki iliyopita na imeathiriwa biashara ya thamani ya karibu dola nusu milioni kwa siku.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Soko la miraa la Beerta lilikuwa bila shughuli wiki iliyopita kufuatia marufuku hiyo

Msemaji wa serikali ya Kenya amesema kuwa marufuku hiyo haikutokana na ziara ya hivi majuzi ya afisa wa cheo cha juu wa kenya, katika eneo lililojitenga nchini Somalia la Somaliland kutafuta soko kwa miraa.

Amesema kuwa Rais Uhuru Kentatta sasa anaingilia kati suala hilo.