Tetemeko la ardhi lakumba Tanzania

Image caption Tetemeko hilo lilisikika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania

Tetemeko la ardhi lenye uzito wa 5.7 katika vipimo vya richa limekumba eneo la Kaskazini Magharibi mwa Tanzania karibu na ziwa Victoria.

Majengo kadha yanaripotiwa kuharibiwa katika miji iliyo karibu.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi za kuwepo maafa . Mitetemeko mingine midogo pia ilisikika katika mataifa jirani ya Kenya na Rwanda.