Man City wawazima Man U nyumbani Old Trafford

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15

Pep Guardiola aliibuka mshindi katika mechi ya kwanza ya lingi kuu nchini Uingezea katika mechi iliyochezwa kati ya Manchester United na Manchester City nyumbani kwa Man U huko Old Trafford.

Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15 alipovamia ngome ya Manchester United na kumpata mlinzi Daley akiwa usingizini.

Raia huyo wa ubelgiji pia alitoa mchango mkubwa katika bao la pili na Man City, baada ya kumpa pasi safi Kelechi Iheanacho ambaye aliutumbukiza mpira wavuni bila kuchelewa.

Iheanacho, mshambuliaji raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 19, alisema anafuraha sana kwa kuipa klabu yake bao la ushindi, na kuongeza imani yake mbele ya meneja Pep Guardiola.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Maurinho na Pep Guardiola