Tetemeko la ardhi lawaua watu 11 Tanzania

Nyumba zilizoporomoshwa na tetemeko la ardhi nchini Tanzania
Image caption Nyumba zilizoporomoshwa na tetemeko la ardhi nchini Tanzania

Maafisa wa Serikali ya Tanzania wanasema kuwa watu 11 wamefariki na wengine karibu 200 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lililokumba Kaskazini Magharibi mwa Taifa hilo.

Wafanyakazi wa kutoa huduma za misaada wanasema watu kadhaa wamekwama katika vifusi kufuatia kuporomoka kwa mijengo kadhaa.

Image caption Tetemeko la ardhi Tanzania

Inadaiwa kuwa hospitali nyingi katika eneo hilo zimejaa majeruhi.

Mitetemeko hiyo ilihisiwa katika mataifa jirani ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Image caption Tetemeko la ardhi Tanzania

Mwandishi wa BBC nchini Tanzania anasema kuwa hilo ndilo tetemeko kubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania kwa zaidi ya mwongo mmoja.