Korea Kusini yaonya kuharibu mji mkuu wa K Kaskazini

Korea Kusini yaonya kuharibu kabisa mji wa Pyongyang
Image caption Korea Kusini yaonya kuharibu kabisa mji wa Pyongyang

Maafisa wa Serikali ya Korea Kusini wamefichua kuwa serikali ina mipango ya kuharibu kabisa mji mkuu wa Korea kaskazini, iwapo ishara yo yote itaonekana kuwa kuna mipango ya kushambuliwa kwa nukilia.

Shirika la Habari la Yonhap lililo na uhusiano mkubwa na Korea Kusini linasema kwamba wabunge nchini humo wamepewa mpango huo.

Mpango huo unanuia kuharibu kabisha makombora yote yaliyo na zana hatari kukiwemo nukilia.

Ufichuzi huu unatokea siku mbili baada ya Korea Kaskazini kulipua angani jaribio kubwa zaidi la kinukilia, ambalo limetoa dhana kuwa Korea Kaskazini imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa zana za kinukilia.