Shambulio la kigaidi latibuliwa Mombasa

Kituo cha police cha Central mjini Mombasa Kenya
Image caption Kituo cha police cha Central mjini Mombasa Kenya

Wanawake watano waliovalia mabuibui na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.

Maafisa wa polisi nchini Mombasa wanasema kuwa walitibua jaribio hilo na kufanikiwa kuwaua wanawake watatu huku wawili wakikamatwa.

Polisi wanasema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kuripoti kuhusu simu ya rununu ilioibiwa.

Na wakati malalamishi yao yalipokuwa yakichukuliwa mmoja wao alichukua kisu na kuwadungu maafisa wawili wa polisi ,huku mwengine akiwarushia polisi waliokuwa wakichukua malamishi hayo bomu la petroli.

Image caption Kituo cha police cha Central mjini Mombasa Kenya

Polisi wanasema kuwa waliwafyatulia risasi na kuwaua wote.

Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.

Image caption Kituo cha police cha Central mjini Mombasa Kenya

Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika eneo la pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni mengi yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab.