Clinton ajuta kuwadharau wafuasi wa Trump

Hillary Clinton na Donald Trump kulia Haki miliki ya picha EPA/AFP
Image caption Hillary Clinton na Donald Trump kulia

Hillary Clinton amesema kuwa anasikitika kuwa aliwataja mashabiki wa mgombezi wa Republican, Donald Trump, kama kundi la watu wasiostahili heshima.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari mgombezi huyo wa Urais kwa chama cha Republican alisema kuwa kuna Wamarekani wengi wanaochapa kazi kwa bidii wanaoamini kuwa wamepuuzwa na wanasiasa nchini.

Hata hivyo alisema kuwa ataendelea kukebehi watu wenye madharau ubaguzi wa rangi.

Meneja Mkuu wa kampeni wa Bwana Trump alikuwa amemlaumu Bi Clinton kwa kile alichokitaja kama matusi dhidi ya mamilioni ya raia wa Marekani aliposema kuwa wale wanaomwunga mpinzani wake walikuwa wabaguzi wa rangi, wapinzani wa kijinsia, maaduni wa wapenzi wa jinsia moja na wanaochukia Waislamu.