Mtu aliyejaribu kumuua Ronald Reagan aachiliwa

Mtu aliyajaribu kumuua rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan aachiliwa huru
Image caption Mtu aliyajaribu kumuua rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan aachiliwa huru

Mtu aliyejaribu kumuua rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, miaka 35 iliyopita, ameachiliwa kutoka hospitali ya watu walio na ulemavu wa akili.

John Hinckley Junior hakupatikana na hatia baada ya kuthibitishwa kuwa alikuwa mlemavu wa akili baada ya kumpiga risasi rais nje ya Hoteli jijini Washington.

Bwana Reagan na watu wengine watatu walijeruhiwa, akiwemo aliyekuwa mkuu ta kitengo cha rais cha habari, James Brady aliyeharibika ubongo.

Kwa zaidi ya miaka 20 sasa hajaathirika na maradhi yake ya akili tena na yeye si hatari kwa maisha ya mtu mwingine tena.

Ataishi kwa mama yake Virginia.

Amekuwa akipelekwa huko kwa siku kadhaa kwa mwezi sasa katika hatua ya kumwandaa kuishi huko maisha yake yaliyosalia.